MAN CITY YAIGARAGAZA HULL CITY NA KUREJEA NAFASI YA PILI EPL


Mchezo wa mwisho katika ligi kuu ya England jana siku ya Boxing ulimalizika kwa ushindi wa bao 3-0 walioupata Manchester City dhidi ya Hull City.

Mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la King Power ilikamilisha idadi ya mechi 8 zilizochezwa siku ya jana.

Licha ya ushindi huo lakini Man City iliwapasa kusubiri mpaka dakika ya 72 kwa Yaya Toure kufungua ubao wa magoli akifunga kwa njia ya penati.

Kelechi Iheanacho alifunga bao la pili na mlinzi Curtis Davis alijifunga kukamilisha ushindi huo wa bao 3-0 walioupata Man City ambao unawarudisha nafasi ya pili katika msimamo.

No comments

Powered by Blogger.