AFRICAN LYON YAIKOMALIA YANGA NA KUTIBUA MIPANGO YOTE


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga imejikuta ikiambulia pointi moja katika mechi yake dhidi ya African Lyon jioni ya leo.


Mchezo baina ya timu hizo ulipigwa katika dimba la Uhuru jijini ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mpaka mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao hivyo kufanya kipindi cha pili kuamua matokeo ya mechi hiyo muhimu kwa Yanga katika kuwania ubingwa.

Dakika ya 59 mchezaji Ludovic Venance aliifungia African Lyon bao la kuongoza baada ya kazi nzuri iliyofanywa na winga wa Lyon akiwachambua na kuwatoka mabeki wa Yanga ambao leo walikua ni Kelvin Yondan, Vicent Boussou,Juma Abdul na Mwinyi Haji.

Amiss Tambwe ndiye aliyeiokoa Yanga dakika ya 74 akifunga bao baada ya mabeki wa Lyon kushindwa kuokoa mpira wa krosi iliyopigwa na beki Juma Abdul.

Katika mchezo huo Yanga ilionekana kabisa kuishiwa mipango na kushindwa kupata  nafasi nyingi za kufunga kama ilivyokua katika mechi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu.

Kwa matokeo hayo Yanga inafikisha pointi 37 katika nafasi ya pili pointi moja nyuma ya Simba wanaoongoza ligi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.