YANGA YAIKIMBIZA SIMBA KIMYA KIMYA, YAICHAKAZA RUVU UWANJA WA UHURU
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara Yanga wameendelea kujiimarisha katika mbio zao za kutetea ubingwa wao kwa kuilaza Ruvu Shooting bao 2-1.
Mchezo huo wa mwisho wa ligi kuu mzunguko wa kwanza ulipigwa jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya kuahirishwa jana.
Ruvu Shooting walitangulia kuliona lango la Yanga kwa goli safi la Abdurahman Musa baada ya kupiga shambulizi la kushtukiza langoni kwa Yanga.
Kazi nzuri iliyofanywa na nahodha wa Yanga leo Haruna Niyonzima kuwachambua mabeki wa Ruvu Shooting na kumtengenezea Simon Msuva ambaye akiwa katikati ya mabeki wa Ruvu Shooting na kuisawazishia Yanga bao hilo hivyo kufanya mchezo huo kuwa sare ya bao 1-1 mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili Yanga walipata pigo baada ya kocha wao Hans Van der Pluijm kutolewa katika benchi na mwamuzi kufatia lugha zisizofaa lakini kipindi hicho hicho Yanga walipata bao la ushindi likifungwa na Haruna Niyonzima baada ya kazi nzuri ya Donald Ngoma.
Kwa matokeo hayo Yanga wanapunguza wigo wa pointi na Simba ambao ni vinara kwa pointi 2 tu, Simba ikiwa na pointi 35 Yanga 33.

No comments