SIMBA WAACHA POINTI TATU MBEYA, AZAM YAUA MWADUI


Vinara wa ligi kuu Tanzania bara Simba wameendelea kupoteza pointi katika mechi zake za kumalizia hatua ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara.


Wakisafiri mpaka jijini Mbeya Simba walishindwa kufurukuta na kujikuta ikilambwa mabao 2-1 kutoka kwa wenyeji Tanzania Prisons.

Jamal Mnyate wa Simba ambaye leo alianza katika kikosi cha kwanza aliipatia Simba bao la kwanza na la pekee kwa wekundu hao ambalo lilipelekea Simba kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Prisons waliamka na kurudisha bao hilo moja na kuongeza bao la pili kupitia kwa Victor Hangaya baada ya udhaifu mkubwa wa mabeki wa Simba.

Hii ni mechi ya pili mfululizo Simba wakipoteza katika ligi kuu baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya African Lyon wakifungwa bao 1-0.

Huko Mwadui Wenyeji Mwadui FC walikubali kichapo cha bao 4-1 toka kwa Wana Lambalamba Azam Fc ya Jijini Dar Es Salaam.

Azam walipata mabao yao kupitia kwa John Bocco,Shaban Idd aliyefunga mabao mawili na Fransisco Zekumbawira.

Bado Simba wanaendelea kuongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 35 wakifatiwa na Yanga wenye pointi 30 ambao kesho watamaliza mzunguko wa kwanza kwa kuvaana na Ruvu Shooting katika uwanja wa Uhuru.

No comments

Powered by Blogger.