SAFARI YA YANGA MBEYA YAANZA KWA KICHAPO,MWAMUZI AVURUNDA
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga wamekutana na kichapo cha pili msimu huu leo kutoka kwa Mbeya City katika uwanja wa Sokoine.
Mchezo huo ambao ulikua wa kasi na wenye vimbwanga vingi ulishuhudia Mbeya City wakiandika bao la kwanza katika dakika ya 6 tu ya mchezo likifungwa na Hassan Mwasapili kwa mpira wa adhabu uliomwacha hoi golikipa wa Yanga Deogratias Munishi.
Wakati Yanga wakiwa katika presha ya kusawazisha bao hilo, Mbeya City waliandika bao la pili kupitia kwa Kenny Ally baada ya kupokea pasi iliyotokana na mpira wa adhabu.
Mwamuzi wa mchezo huo Rashid Mrope alitoa kali ya mwaka baada ya kufanya maamuzi ya aina tatu kuhusu bao hilo. Yanga walililalamiakia bao hilo la pili wakidai lilifungwa wakati mwamuzi akiwaonesha mabeki wa Yanga mahali pa kuweka ukuta wao.
Mwamuzi akiwa tayari amekwishakubaliana na bao hilo, aliamua kusikiliza malalamiko ya nahodha wa Yanga Haruna Niyonzima, akabadili uamuzi kwa kusema mpira huo wa adhabu urudiwe kupigwa.
Mbeya City hawakukubali na halmanusura mchezo huo uvunjike baada ya wachezaji wa Mbeya City kutoka uwanjani wakilalamikia uamuzi mbovu wa mwamuzi huyo kutokea Ruvuma.
Baada ya Mbeya City 'kukaza' ndipo mwamuzi alipoamua kubadili kauli na kulikubali goli hilo lililofanya ubao kusomeka 2-0.
Baada ya dakika 45 kukamilika, mwamuzi wa mezani alionesha nyongeza ya dakika 4, lakini kitu cha kushangaza ni kwamba kipindi hicho kilikwenda mpaka dakika ya 52 ikiwa ni nyongeza ya dakika 7.
Katika dakika hizo za nyongeza, Yanga walifanikiwa kuandika bao la kufutia machozi lililofungwa na Donald Ngoma wakitumia vyema mpira wa 'Fair Play' kutoka kwa mwamuzi.
Kipindi cha pili kilikua cha piga nikupige huku Mbeya City wakikitumia sana kupoteza muda na Yanga wakijitahidi kusawazisha.
Mpaka mwisho wa mchezo huo ambao mwamuzi alishindwa kabisa kuumudu, matokeo yalikua ni Mbeya City 2-1 Yanga.
Yanga iko jijini Mbeya kwa michezo miwili ya ligi kuu ya soka Tanzania bara ambapo wikiendi itacheza na Tanzania Prisons katika dimba hilo hilo la Sokoine
Kwa matokeo hayo Yanga imeendelea kukamata nafasi ya pili na pointi zao 27 lakini sasa ikiachwa pointi 8 na vinara Simba ambao leo waliitandika Stand United bao 1-0

No comments