RONALDO APIGA HAT-TRICK AKIVUNJA NA KUWEKA REKODI MPYA LA LIGA
Cristiano Ronaldo jana usiku aliingia katika rekodi nyingine baada ya kuiongoza Real Madrid kuibuka na ushindi dhidi ya majirani zao Atletico Madrid.
Mchezo huo wa La Liga ulipigwa katika dimba la Vicente Calderon nyumbani kwa Atletico Madrid ulishuhudiwa Real Madrid wakiibuka na ushindi wa bao 3-0.
Cristiano Ronaldo ndiye aliyefunga magoli yote hayo matatu la kwanza akifunga kipindi cha kwanza na mawili ya kipindi cha pili moja likiwa la penati, lingine la adhabu ndogo na la mwisho akiunganisha krosi ya Gareth Bale.
Ronaldo kwa magoli hayo mamkon ambayo ni hat-trick yake ya 39 tangu ajiunge na Real Madrid, amevunja rekodi ya mkongwe Alfredo di Stefano iliyodumu miaka mingi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli mengi zaidi katika mechi zilizohusisha Real na Atletico Madrid akiwa na magoli 18 na kuyazidi yale 17 ya Alfredo di Stefano.
WAFUNGAJI BORA KATIKA MADRID DERBY
● Cristiano Ronaldo - 18
● Alfredo di Stefano - 17
● Santillana -15
● Puskas - 13
● Campos - 12

No comments