LIGI KUU ENGLAND JANA: CHELSEA YAIFUMUA EVERTON NA KUSHIKA USUKANI,MAN CITY YABANWA, SUNDERLAND YAFUFUKA
Chelsea ndiyo vinara wa ligi kuu nchini England kwa sasa baada ya jana kuifumua Everton kwa bao 5-0 katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge jijini London.
Eden Hazard alifunga bao 2, beki Marcos Alonso,Pedro Rodriguez na Diego Costa wote walifunga bao 1 kila mmoja katika ushindi huo mnono kwa kocha Antonio Conte na kuiwezesha kukamata usukani wa ligi hiyo ikifikisha pointi 25.
Sunderland wao baada ya kuhangaika sana kupata ushindi katika ligi kuu jana waliweza kupata ushindi wa kwanza tena wakiwa ugenini wakiifunga Bournemouth bao 2-1 magoli ya Victor Anichebe na Jermaine Defoe yalitosha kumpa ahueni kocha David Moyes.
Manchester City wakiwa nyumbani walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Middlesbrough katika dimba la Etihad. Goli la mapema la Sergio Aguero likizimwa na goli la dakika za mwisho la Marten De Doon na kuinyima City kukwea katika msimamo wa ligi hiyo.
West Ham wakiwa nyumbani walitoka sare ya bao 1-1 na Stoke City wakati Burnley wakiibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Crystal Palace.

No comments