BAYERN MUNICH HOI KWA DORTMUND YAPOKONYWA UONGOZI BUNDESLIGA
Mabingwa watetezi wa Bundesliga Klabu ya Bayern Munich jana walionja kipigo cha kwanza msimu huu kwa kufungwa bao 1-0 na Borussia Dortmund.
Pierre Emenike-Aubemeyang mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon aliifungia Dortmund bao pekee dakika ya 11 tu ya mchezo bao lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.
Ushindi huo wa bao 1-0 katika uwanja wa Signal Induna ni wa kwanza kwa Dortmund dhidi ya Bayern Munich tangu mwaka 2012 katika Bundesliga.
Bayern Imepoteza nafasi ya kurudi katika uongozi wa ligi hiyo baada ya kushindwa kuwafikiwa vinara RB Leipzig ambao Ijumaa walishinda 3-2 na kukwea kileleni mwa msimamo wakifikisha pointi 27 huku Bayern Munich wakibaki na pointi zao 24 na Dortmund wao wanapanda mpaka nafasi ya 3 wakiwa na pointi 21.

No comments