VPL: YANGA YAICHAKAZA TOTO,AZAM SARE, STAND YABONDWA MBEYA

Mzunguko wa 11 wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliendelea tena jana kwa mechi 6 kuchezwa katika viwanja mbalimbali hapa nchini.


Mabingwa watetezi Yanga wakiwa ugenini kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza iliweza kuwalaza wenyeji Toto African ya huko kwa bao 2-0.

Magoli ya Yanga yalifungwa na Obrey Chirwa kwa kichwa akiunganisha krosi ya Simon Msuva kisha Msuva akafunga bao la pili kwa njia ya penati baada ya beki wa Toto African kumwangusha Deus Kaseke eneo la hatari.

Huko jijini Mbeya rekodi ya Stand United kutofungwa msimu huu iliishia kwa maafande wa Prisons baada ya kuchapwa bao 2-1 Katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la  Sokoine jijini Mbeya.

Hapa Dar es Salaam wenyeji Azam FC wakiwa katika dimba Lao la nyumbani walilazimishwa  sare ya bao 1-1 mchezo uliopigwa majira ya Saa 1 kamili jioni, Mtibwa wakitangulia kufunga kupitia kwa Rashid Mandawa kabla ya Himid Mao hajasawazisha kwa njia ya penati.

Maji Maji wakisahau matokeo mabaya ya mwanzo wa msimu waliendeleza matokeo mazuri wakiwa na  Kocha wao Mpya Kally Ongala  baada ya kuwalaza African Lyon bao 2-0 mchezo uliopigwa katika dimba la Uhuru jijini.

Huko Kibaha wenyeji Ruvu Shooting walilazimishwa sare ya bao 1-1 na Mwadui toka Shinyanga.

Ndanda FC wao wakiwa nyumbani walishindwa kulinda goli Lao la mapema walilopata dhidi ya Mbeya City baada ya kuruhusu bao la kusawazisha ikiwa imebaki dakika 1 mpira kumalizika hivyo mpira kuisha kwa sare ya bao 1-1.

Ligi hiyo itaendelea tena Leo kwa Simba ambao ni vinara kuwaalika Mbao FC ya Mwanza katika dimba la Uhuru.


No comments

Powered by Blogger.