SINTOFAHAMU YA KUKODISHA IMESHIKA KASI, SASA YANGA WAITANA KWA DHARURA.

Kuna vuguvugu linaendelea katika klabu ya Yanga baada ya mchakato wa kuikodisha klabu hiyo kwa kampuni iitwayo Yanga Yetu kutotambuliwa na Baraza la michezo la taifa BMT.


Uchunguzi uliofanywa na www.wapendasoka.com umebaini kwamba kuna mkinzano baina ya wanachama wa klabu hiyo kati ya wale wanaounga mkono mabadiliko hayo na wale wasiotaka hata kusikia mambo hayo.

Sasa taarifa ambayo imetufikia hivi karibuni ni kama ifuatavyo...

Klabu ya Yanga inapenda kuwatangazia wanachama wote wa Young Africans Sports Club (YANGA)  kuwa patakuwa na mkutano mkuu wa dharura siku ya jumapili ya tar 23/10/2016.

Wanachama wote mnaombwa kufika bila kukosa kwani ni kwa faida na maslahi mapana ya Timu yetu.

Agenda za mkutano pamoja na mahali mkutano mkuu utakapofanyika mtajulishwa mapema kabla ya siku husika kufika.

'YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO'

Imetolewa na Uongozi - Young Africans Sports Club.

No comments

Powered by Blogger.