SAKATA LA MASHABIKI KUNG'OA VITI UWANJA WA TAIFA,SIMBA YALIMWA FAINI
Vinara wa ligi kuu Tanzania bara Simba wamepigwa faini ya shilingi milioni 5 kufuatia fujo za mashabiki wake katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya watani zao Yanga.
Faini hiyo imekuja siku chache baada ya Serikali kutangaza kuzifungia timu hizo mbili kutumia uwanja wa Taifa kutokana na mashabiki wake kufanya vurugu na kupelekea uaribifu wa miundo mbinu ya uwanja hasa viti vya kukalia mashabiki.
Pia Afisa habari mkuu wa klabu hiyo (Simba) Haji Manara amekumbana na faini ya laki 2 kufatia kuingia uwanjani baada ya mchezo wakati hakuruhusiwa kuingia wala hakuwa mmoja wa maofisa waliopaswa kuingia.
Kikao cha kamati ya bodi ya Ligi kilichoketi jana Jijini Dar es Salaam pia kimeipiga faini ya milioni 3 klabu ya Azam FC kufatia kuvaa upande mmoja tu katika jezi nembo ya mdhamini wa ligi hiyo.
Swala la Refa Martin Saanya halijatolewa maamuzi rasmi kwani Kamati inaendelea na uchunguzi ila Kadi nyekundu ya Jonas Mkude imefutwa rasmi.
Nakala ya barua ya TFF hii hapa
No comments