FUATILIA HAPA KINACHOENDELEA YANGA KUHUSU KOCHA HANS VAN DER PLUIJM
LWANDAMINA AKANA KUZUNGUMZA NA YANGA
Kocha Mzambia George Lwandamina ambaye amekua akihusishwa kwa kiasi kikubwa na kujiunga na Yanga amekana kufanya mazungumzo na mabingwa hao wa Tanzania Bara.
Lwandamina amesema yupo nchini kwa shughuli zake za kibiashara na hajaletwa na Yanga kama wengi wanavyodhani.
"Tanzania siyo ya Yanga peke yake, kuna vitu vingi vya kufanya hapa kwa sababu Tanzania ni mahali pazuri kwa shughuli za kiuchumi"
"Mara ya mwisho nilipata ofa kutoka Afrika Kusini lakini sikuwenda, kwa hapa Tanzania sijapata ofa."
******************************
Uongozi wa Yanga umetoa taarifa kwamba unasikitika kwa maamuzi aliyoyachukua Mwalimu Hans Van De Pluijm, lakini wameheshimu maamuzi yake ya kujiuzulu nafasi ya Kocha Mkuu wa Young Africans Sports Club. Yanga imekubali maamuzi hayo na inamtakia kila la kheri huko aendako.
Taarifa zaidi za kujaza nafasi hiyo zitatolewa.
*******************************
Kocha Hans Van Pluijm amethibitisha kwamba amejiuzulu kuifundisha Yanga kwa sababu ambazo hakutaka kuziweka wazi japo haashirii kama amejiuzuru kwa sababu za kupendeza.
"Ni kweli, nimejiuzulu kuifundisha Yanga, tayari nimewasilisha barua yangu kwa klabu na mambo mengine unaweza kuiuliza klabu"
"Nawashukuru sana mashabiki wa Yanga kwa ushirikiano wao, ninawaheshimu sana na ninawaokba radhi kwa hatua hii niliyoamua kuichukua"
******************************
Taarifa nyingine ambayo imetufikia inasema kocha msaidizi Juma Mwambusi ataendelea kukinoa kikosi cha Yanga mpaka kocha mpya atakapoanza kazi November 1. Endelea kuifuatilia wapendasoka.com
******************************
Kwa mujibu wa Meneja Hafidh Saleh, si kweli kwamba benchi zima la ufundi limejiuzulu, yeye binafsi hajaandika barua ya kujiuzulu wala hajapata taarifa yoyote kutoka kwa uongozi wa Yanga.
"Siyo kweli, hizo ni taarifa za kupikwa na mimi nazisikia tu kwenye vyombo vya habari kwamba eti sisi tumepeleka barua za kujiuzulu"
"Mimi na kocha Mwambusi tupo kazini tunajiandaa na mechi ya keshokutwa na hatujapata taarifa yoyote kutoka kwa uongozi"
********************************
Taarifa zinazidi kumiminika, Inayotufikia sasa hivi ni kwamba benchi zima la ufundi la Yanga limejiuzulu.
Anayetajwa kuchukua nafasi ya meneja ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo Sekilojo Chambua, japo mwenyewe amekana kupokea taarifa yoyote.
********************************
Kumekuwa na taarifa za ujio wa kocha mpya George Lwandamina kutoka Zambia ambaye alifika nchini jana lakini viongozi wa Yanga wamekua wakizikanusha na kusisitiza kwamba Pluijm baso ni kocha wao japo taarifa ya uhakika ni kwamba
Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema tayari barua ya Pluijm imepokelewa na uongozi umeridhia kujiuzulu kwake.
Taarifa zaidi endelea kuitembelea wapendasoka.com
No comments