NI MWAKA WA KICHUYA, ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI SEPTEMBER.


Nyota ya Shiza Ramadhan Kichuya wa Simba imezidi kung'ara katika anga za soka Tanzania baada ya mashabiki wa klabu yake ya Simba kumpigia kura nyingi za mchezaji bora wa mwezi September.

Habari ambazo wapendasoka.com ilizipata punde tu baada ya kura ambazo hupigwa kupitia ukurasa wa klabu ya simba kuhesabiwa zinasema Kichuya ndiye kinara wa tuzo hiyo kwa mwezi Septemba.

Kichuya anatarajiwa kutangazwa rasmi mchana wa leo kabla ya kukabidhiwa tuzo yake na kitita cha sh 500,000/- katika uwanja wa Uhuru kabla ya mchezo wa ligi kuu ambao Simba watawakaribisha Kagera Sugar.


Kichuya anakua mchezaji wa pili kushinda tuzo hiyo msimu huu baada ya beki Mohamed Hussen kunyakua tuzo ya mwezi Agosti.

Aidha Kichuya anaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kunyakua hata tuzo ya mwezi October kutokana na ukweli kwamba ndiyo mwezi ambao ameng'ara zaidi akiwafunga watani wa jadi Yanga bao la kona iliyotinga kimiani moja kwa moja.

No comments

Powered by Blogger.