MCHAKA MCHAKA LIGI KUU WIKIENDI HII
Uhondo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17, raundi ya 12 unaendelea kesho Jumamosi kwa michezo sita.
Mabingwa watetezi Yanga watakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye kapeti jipya la uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Uhuru African Lyon watawakaribisha Mbeya City ya Mbeya katika mchezo ambao utaanza saa 8:00 mchana wakati wachimba madini wa Mwadui kutoka Shinyanga wakisafiri hadi Mtwara kucheza na wanakuchwele Ndanda Fc kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Wapiga debe wa Stand United watatembelea katikati ya mashamba ya miwa huko Manungu Turiani Morogoro kuzitafuta pointi tatu mbele ya wakata miwa wa Mtibwa.
Majimaji ambao siku hizi siyo tena wa mchezo mchezo watakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wao wa Majimaji huko Songea.
Huko Azam Complex Chamazi matajiri wa lamba lamba na mikate Azam FC watajaribu kujitutumua nyumbani mbele ya JKT Ruvu kuanzia saa 1.00 usiku.
Jumapili itakuwa ni zamu ya vinara wa ligi hiyo, Simba ambao wataikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Uhuru wakati wajela jela Tanzania Prisons wakiwa nyumbani kuwaalika wachana mbao wabishi Mbao FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Shirikisho la soka Tanzania TFF linasisitiza kwamba Michezo yote ya Dar es Salaam, mfumo wa kuingia utabaki kuwa ni uleule wa kutumia kadi za Selcom kununua tiketi za kielekroniki.
Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa Uhuru ni Sh 30,000 kwa Jukwaa Kuu (VIP-A), VIP-B na C Sh 20,000 na mzunguko ni Sh 5,000 wakati Kiingilio Uwanja wa Azam ni Sh 10,000 kwa VIP na Mzunguko ni Sh 3,000.

No comments