MAOURINHO AMREJESHA SCHWEINSTEIGER KIKOSINI MAN UNITED

Hatimaye kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameamua kumrejesha kikosini kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger baada ya miezi minne nje ya kikosi.



Mwanzoni mwa msimu huu Kocha Jose Mourinho alinukuliwa akisema kwamba nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani hatakua na nafasi katika kikosi chake na kumpeleka kufanya mazoezi na kikosi cha pili lakini leo ameonekana katika uwanja wa mazoezi AON akifanya mazoezi na wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza.

Pamoja na Bastian Beki Phil Jones pia ameonekana akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Bado haijajulikana kama Huu ni mwanzo kwa kocha Jose Mourinho kumrudisha kikosini nyota huyo au hapana na mkataba wake utamalizika mwaka 2018.







No comments

Powered by Blogger.