KUELEKEA KATIKA MECHI YA LIVERPOOL NA MAN UNITED HAYA HAPA MAMBO 11 UNAYOPASWA KUYAFAHAMU

□ Kama Liverpool itafungwa leo itakua mara ya kwanza katika historia kupoteza michezo mitatu mfululizo katika ligi kuu wakiwa nyumbani dhidi ya Manchester United Tangu mwaka 2005.

 □  Manchester United wameshinda katika mechi  7 kati ya 9 zilizopita katika ligi dhidi ya Liverpool.

□ Liverpool wamepoteza mechi 67 za ligi walizocheza dhidi ya Manchester United hakuna timu yoyote iliyoweza kuifunga Liverpool mechi nyingi kiasi hicho.

 □ Liverpool na Manchester United hazijawahi kutoka sare tangu mwezi Octoba 2011 walipotoka sare ya bao 1-1.

□ Steven Gerrard ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika michezo inayokutanisha timu hizo akifatiwa na Wayne Rooney na Robbie Fowler ambao wote wana magoli 6.

□ Liverpool kama wakishinda leo watakua wameshinda mechi ya 5 mfululizo katika ligi msimu huu na itakua mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo mwezi Machi mwaka  2015.

□ Jurgen Klopp amepoteza mchezo mmoja tu katika michezo mitano dhidi ya Jose Mourinho akishinda mara 3 na kutoka sare mara 1.

□ Kikosi cha Man United chini ya Jose Mourinho kimeshinda mechi moja tu katika mechi 4 zilizopita katika ligi kikifungwa goli 7.

□  Wayne Rooney mpaka sasa ana magoli 87 katika ligi kuu ambayo amefunga akicheza katika viwanja vya Ugenini akiwa ni mchezaji wa pili kuwa na magoli mengi ya ugenini mwingine ni Alan Shearer.

□ Manchester United walikua na pointi 3 zaidi (Pointi 16) muda kama huu msimu uliopita wakiwa chini ya kocha Louis Van Gaal.

□ Marcus Rashford amefunga magoli 12 tangu alipocheza mchezo wa kwanza kwa Man United ikiwa ni magoli manne zaidi ya mchezaji yoyote katika kikosi cha Manchester United.

No comments

Powered by Blogger.