JOHN TERRY AWAPASHA WANAOMZOMEA WAYNE ROONEY

Baada ya kuzomewa na mashabiki katika mechi dhidi ya Malta na kupelekea kutemwa katika kikosi cha England kitakachoivaa Slovenia leo mambo mengi yameendelea kusemwa kuhusu nahodha Wayne Rooney.


John Terry ambaye ni nahodha wa zamani wa England amefunguka na kuwakosoa wote wanaompondea Wayne Rooney na kupitia katika ukurasa wake wa Instagram Terry aliandika haya

"Wayne Rooney ni mfungaji bora kabisa katika historia ya timu ya Taifa ya England.
Bado mechi chache atakua mchezaji pekee aliyecheza mechi nyingi zaidi akiwa na timu ya taifa ya England"

 "Ni mmoja kati ya wachezaji bora kabisa niliowahi kuwaona na kubahatika kucheza nao mtu ambaye alijitolea kila kitu kwa ajili ya Timu ya taifa ya England"

"Mchezaji bora na wa mfano wa Everton Manchester United,England na ulimwengu wa Soka"

"Tunapaswa sote kumpa heshima yake mchezaji huyu na kuwa nyuma yake na kikosi chetu cha England" Alimaliza kusema John Terry.

Tayari Wayne Rooney alishatangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa ya England mwaka 2018 lakini kwa kinachoendelea hivi sasa yawezekana ikasababisha mchezaji huyo akastaafu mapema.

Jordan Handerson amepewa jukumu la kuiongoza England dhidi ya Slovenia leo wakati Eric Dier akichukua nafasi ya Wayne Rooney kama kiungo mkabaji.

No comments

Powered by Blogger.