JE UNAJUA ULIPOANZIA UPINZANI WA MANCHESTER UNITED NA LIVERPOOL? SOMA HAPA

MANCHESTER UNITED VS LIVERPOOL Hili ni pambano kubwa zaidi kwenye historia ya soka la England na ni moja kati ya michezo inayotazamwa na watu wengi  sana duniani.



Jumatatu ya Oktoba 17 timu hizi zitakutana kwa mara ya kwanza katika mchezo wa ligi kuu ya England katika dimba la Old Trafford na hapa nimekuwekea baadhi ya mambo machache kuelekea mechi hii

1. Mechi ya kwanza kati ya vigogo hawa ilikua 18/4/1894 ambapo liverpool waliibuka na ushindi wa magoli 2-0

2. Livepool wameshinda goli 7 mara mbili dhidi ya manchester mwanzo ikiwa msimu wa 1907/1908 ambapo walishinda 7-4 na mwaka 1985 ambapo walishinda 7-1 vipindi ambavyo liverpool walikua wanatawala soka la dunia. Manchester walilipa kisasi mwaka 1927 kwa kushinda 6-1

3. Ryan Giggs ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi kati ya wachezaji waliocheza mechi hizi akicheza mechi 48 akifunga mara 5 huku Steven Gerrard akifunga magoli mengi magoli 9 (5 yakiwa ni ya penati)

4. Mwaka 1946 baada ya vita ya pili ya dunia Old Trafford iliharibiwa vibaya hivyo Manchester United na Manchester City walikua wakitumia uwanja mmoja ambao ulimilikiwa na Manchester City na kwenye pambano dhidi ya Liverpool Manchester United iliwafunga mashabiki wa timu zote mbili (Man City na Liverpool) walioungana dhidi ya Manchester United...
Man United ilishinda 5-0 huku legend wa Manchester United Stan Pearson akifunga hat-trick.

5. Moja kati ya wachezaji pendwa wa manchester sir matt busby alichezea zaidi ya mechi 100 livepool huku pia akicheza man city na angeweza kua kocha wa liverpool ila baada ya manchester kugundua ilibidi wampe wao timu haraka haraka na akaitumikia united badala ya city

6. Liverpool haijawahi kukosa matokeo mara 5 mfululizo na Manchester United kwenye ligi na jinsi ilivo Liverpool hajapata ushindi kwenye mechi nne za ligi dhidi ya Manchester United

UPINZANI ULITOKA WAPI ?


Upinzani wa hizi timu mbili ni zaidi ya upinzani wa mpira huu ni upinzani wa miji, uchumi, ukuaji wa sekta za kiselikali na viwanda....

Upinzani huu ulianza karne ya 18 ambapo Manchester ulikua mji mkubwa Uingereza ukitoa London ghafla Liverpool wakapata bandari na kuanza kukua kwa kasi kiasi ikaipiku Manchester na kua mji mashuhuri huku serikali ikiipendelea Liverpool kupeleka huduma mbali mbali kiasi zilivokuja hizi timu mbili ilikua chachu ya upinzani kati ya miji hii miwili iliyopo na tofauti ya km 56 tu.

Miaka zaidi ya 100 baadae upinzani huu umekua mkubwa kiasi timu hizi mbili zimeandika barua kwa mashabiki wake kutofanyiana fujo kama ilivokua kwenye mechi ya mwisho ya Europa League.

Hii ni mechi kubwa zaidi duniani amini usiamini ni zaidi ya mpira kiasi Kocha Sir Alex Ferguson alivyopewa timu alisema " kazi yangu kubwa sio kuipandisha juu Manchester United kazi yangu kubwa ni kuitoa Liverpool out of their fu*** perch..." Mzee alitukana hahahaha.

Ameandika WeAllove Hoff  (member: Wapenda Soka Facebook group)


No comments

Powered by Blogger.