HIKI NDICHO KILICHOTOKEA KATIKA LIGI KUU ENGLAND JANA (+Video highlights)

Ligi kuu iliingia mzunguko wake wa tisa kwa mechi nane jana jumamosi 22/10/2016.




● AFC Bournemouth imetoshana nguvu na Tottenham Hotspur kwa sare ya 0-0 ikiwa nyumbani katika mchezo wa mapema kabisa hiyo jana.

Kiungo Mousa Sissoko anaweza kua matatani baada ya kuonekana akimpiga kiwiko Arter ambaye aliibuka kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

Kiungo Jack Wilshire anayeichezea Bournemouth kwa mkopo akitokea Arsenal alicheza dakika zote 90 kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu.

● Mabingwa Leicester City waliichapa Crystal Palace bao 3-1. Leicester City ilikua na matokeo mabaya ikipoteza michezo yake miwili ya nyuma kabla ya ushindi huo wa jana.

Ahmed Musa,Shinji Okazaki na Christian Fuchs ndiyo walioipa ushindi huo mnono Leicester City

Angalia highlights hapa


● Arsenal wakiwa nyumbani ikiwa ni Birthday ya kocha wao Arsene Wenger walijikuta wakipunguzwa kasi na Middlesbrough kwa sare ya bila kufungana.



● swansea Ikiwa nyumbani ilitoka sare ya bila kufungana na Watford ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa kocha Bradley wa Swansea katika uwanja wa Liberty.

● Liverpool wakiwa nyumbani waliifunga West Brom kwa bao 2-1 magoli ya Sadio Mane na Philip Coutinho huku Gareth McAuley akiipatia West Brom goli la kufutia machozi.

Angalia highlights hapa


Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa mechi mbili

3:30 PM - Manchester City vs Southampton
6:00 PM - Chelsea vs Manchester United

~Abel Alvaro

No comments

Powered by Blogger.