YONDANI "AIKACHA" SAFARI YA TAIFA STARS NIGERIA
Sentahafu
wa Young Africans, Kelvin Yondani si miongoni mwa wachezaji 18 walioondoka leo
Septemba mosi, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa hatua ya
makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON
2017).
Taarifa ambazo Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) imezipata ni kwamba Yondani ana matatizo ya kifamilia
ambako hajayaweka sawa hadi timu hiyo inaondoka kwenda Nigeria na Kocha Mkuu wa
Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa hajajaza nafasi hiyo.
Mkwasa amekerwa na kitendo hicho,
lakini TFF itasubiri ripoti ya kocha huyo mara baada ya kurejea kutoka Nigeria.
Timu hiyo imeondoka na wachezaji 18
huku ikitarajiwa kuungana na na Nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta nchini
Nigeria. Samatta - Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea timu ya
Genk ya Ubelgiji anatokea jijini Brussels ambako makocha wake wamemwomba Mkwasa
na Daktari wa Taifa Stars, Richard Yomba kumwangalia namna ya kumtumia kwa
sababu ya uchovu wa mechi nzito zilizoipa matokeo mazuri ya kutinga hatua ya
makundi ya Uropa Ndogo.
Taifa Stars inakwenda Nigeria kwa
ajili ya mchezo huo dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles
utakaofanyika Septemba 3, 2016.
Licha ya mchezo huo kuwa sehemu ya
mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon,
lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kwa fainali hizo
kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo
iliyojitoa katikati ya mashindano.
No comments