YANGA KUENDELEA KUWAKOSA NYOTA HAWA KESHO

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga kesho watajitupa katika mchezo wao wa tatu wa ligi kuu msimu huu.


Yanga kesho kwa mara ya kwanza itaanza kuutumia uwanja wa Uhuru watakapoikaribisha Maji maji ya Songea katika mchezo wa tatu kwa Yanga baada ya kulazimishwa sare na Ndanda katika mchezo uliopita.

Katika mchezo wa kesho Yanga itaendelea kuwakosa nyota wake kadhaa wakiwemo Vicent Bousou na Haruna Niyonzima ambao walikua na timu zao za taifa wakati Mbuyi Twite,Geoffrey Mwashiuya na Deo Munishi wameanza mazoezi leo baada ya kuwa majeruhii huku Dida akitoka katika msiba wachezaji hao ni hati hati kuanza katika mchezo wa kesho.



No comments

Powered by Blogger.