VIGOGO WA YANGA WAIFUATA TIMU YAO KAMBINI PEMBA

Muda wowote ule kabla ya siku kumalizika Yanga wataingia Dar es Salaam kwa usafiri wa ndege wakitokea Pemba ambako waliweka kambi ya kujiwinda na mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Simba.


Kabla ya kuwasili leo, Wadau matajiri wa klabu hiyo hawakutaka kusubiri, waliamua kuruka kwa ndege ya kukodi jana hadi Pemba ambako walifanya mazungumzo nyeti sana na wachezaji juu ya mchezo unaowakabili.

Habari zisizokua na tone la shaka ambazo wapendasoka.com imezipata zinasema pamoja na mengine waliyokua nayo vigogo hao, muhimu ni ahadi ya fedha kiasi cha shilingi milioni 20 iwapo watamuua mnyama uwanjani Taifa kesho.

Huenda mambo yakazidi kuwa mazuri kwa wachezaji wa Yanga kwa sababu mara baada ya kuwasili leo watakua na mazungumzo na Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji ambaye bado haijaeleweka anataka kuzungumza nini lakini historia haioneshi kwamba anaweza kuwaacha hivi hivi

No comments

Powered by Blogger.