MSHAMBULIAJI MAN CITY AIMALIZA TAIFA STARS NIGERIA
Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria anayeichezea Manchester City ya England Kelechi Iheanacho jioni hii ameifungia Nigeria bao pekee katika mchezo dhidi ya Taifa Stars.
Mchezo huo wa kukamilisha Ratiba ya Michezo ya kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani huko Gabon.
Mchezo huo wa kundi G uliopigwa katika mji wa Uyo huko Nigeria ulishuhudia mechi kali iliyotawaliwa na uimara wa kila upande hasa upande wa Stars kipa Aishi Manula ambaye aliokoa michomo mingi ya maana mpaka dakika ya 79 Nigeria walipopata bao pekee.
Kwa matokeo hayo Misri imebaki na pointi zake 10 Nigeria wakwa na pointi 5 nafasi ya pili wakati Stars wanakamata nafasi ya mwisho wakiwa na pointi 1.
Katika mchezo huo Nigeria ilichezea wachezaji wake wote wakali wanaocheza katika ligi mbalimbali ikiwemo ligi kuu ya England Ahmed Musa,Kelechi Iheanacho,Victor Moses na Obi Mikel.
Nigeria wakitoka uwanjani wakati wa mapumziko |

No comments