MAMBO NILIYOYAONA KWENYE MECHI ZA ARSENAL MSIMU HUU.

Na Martin Kiyumbi


1: Tunaweza tukawa sahihi kuyashambulia maamuzi ya Arsene Wenger kumchezesha Sanchez kama mshambuliaji wa kati, lakini kwa Wenger anaweza akawa ameona zaidi tena kwa kutokutumia macho ya nyama. Hakutumia macho ya nyama kumtengeneza Henry kuwa mshambuliaji wa kati tishio kutoka kwenye ushambuliaji wa pembeni nafasi aliyokuwa anacheza awali.
Kwa Sanchez pia anajaqribu kufanya hivyo lakini kuna vitu ambavyo Sanchez anavikosa.Kwanza anapoteza mipira sana, pili hawezi kukabiliana na beki uso kwa uso (Yeye akiwa na mpira beki akiwa mbele yake), kitu kizuri kwa Sanchez ana weza kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga, na kupiga pasi za mwisho kama ilivyokuwa kwa Henry.

2:Kitu kinachoitofautisha Arsenal ya msimu huu na Arsenal ya misimu miwili iliyopita ni hiki hapa, Misimu miwili iliyopita Wakati Coquelin akiumia katikati ya mechi Chambers ndiye aliyekuwa ananyanyuka kwenye benchi kwenda kuziba pengo lake. Msimu huu ni tofauti sana, kuna wachezaji wawili wa kiwango kizuri wapo kwenye benchi kwa ajili ya nafasi yake (Xhaka na Mud).
Wenger hakuridhika na ujio wa Mud msimu uliopita , msimu huu akamuongeza Xhaka ambaye amezidi kuing’arisha taswira ya Arsenal. Nafasi hii wanayocheza kina Coquelin, Xhaka na Mud ndiyo nafasi ambayo siku zote ikiwa vizuri kwenye kikosi cha Arsenal ya Wenger basi Arsenal ndipo uonekana hai, Tangia enzi za Vieira, alipotoka Arsenal wakaingia rasmi kwenye njia yenye giza, akaja Flamin , baada ya Flamin kutoka ndipo Arsenal ikaingia gizani rasmi, lakini kwa sasa Mwanga unaonekana.

3: Kwa misimu mingi iliyopita Arsenal imekuwa ikicheza mechi 40 kwenye ligi ya EPL, mechi nyingi kuzidi timu zote shiriki za EPL, hii ni kutokana na kukutana mara mbili kwa msimu na timu inayoitwa majeruhi na mara zote Arsenal ilikuwa ikipoteza .Majeruhi yamekuwa yakiwaathili sana na kuzingatia kuwa kila mchezaji muhimu aliyekuwa anaumia hakukuwepo na mchezaji mzuri ambaye angeziba pengo lake hata kwa nusu ya ubora wake. Msimu huu tumeshamsahau Ramsey kwa sababu kwenye sehemu yake hatuoni mwanya, Gabriel yupo kwenye mbao kumsaidia Kosciely, Holding yuko kwa ajili Mustafi, Umri wa Holding usikuogopeshe ila ogopa akicheza bila kiongozi kule nyuma.

Maana halisi ya kuwa na kikosi kikubwa si kuwa na wachezaji wengi ila ni kuwa na wachezaji wanaokaribiana viwango vya uchezaji au kulingana kwenye kila nafasi uwanjani na kwa hapa Arsenal imefanikiwa kwa 80% kiwango ambacho kinatosha kushinda dhidi ya timu ya majeruhi.

4: Unataka nimzungumzie Iwobi ? Bila shaka yeye ni mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Arsenal, sitaki kuizungumzia njaa na hamasa yake aliyonayo kuhusu mafanikio kwa maana haifichiki hata kwa upole wake miguu yake huelezea zaidi kuliko andishi langu lolote nitakalo lileta, zitazame pasi zake za mwisho za magoli , tazama anavyohusika kwenye upatikanaji wa magoli kwenye kila mechi, hana mbio za kumzidi OX , hana vyenga vya maudhi, yeye anajua kushambulia kwa nguvu, kutoa pasi vizuri hasahasa pasi za mwisho, anajua kufunga, hapotezi mipira ovyo, anajua kukaa kwenye nafasi yake, anakaba pale timu inapokuwa haina mpira, unahitaji nini tena kutoka kwa mchezaji wa aina hii tena mwenye umri mdogo?

 Hiki ni kitabu sahihi kwa Ox cha kujifunzia.Akiona kina lugha ngumu basi nitamletea chenye lugha ya kijerumani cha mwandishi Gnabry ambaye yeye alistahili kukaa pale Arsenal na OX kutokuwepo pamoja na Ozil kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Iwobi anahitaji kuimarisha nidhamu yake ya mpira kufikia ukomavu haswaa wa kiuchezaji,bado ana mengi ya kujifunzana uzur umri wake unamruhusu sana.

5: Njia sahihi ya Arsenal kujilinda ni wao kumiliki mpira, Ni hatari sana kwa Arsenal inapokuwa inajilinda kwa kumkaribisha mpinzani kwani hushambuliwa kwa nguvu na pressure huwa ndani ya wachezaji wa Arsenal. Lakini ni tofauti na pale Arsenal inapokuwa inaongoza hata goli moja na bado ikaendelea kumiriki mpira kwani pressure kwao hupungua sana, nah ii ndiyo njia sahihi kwao kwa kujizuia. Niliwaona kwenye mechi dhidi ya PSG na Chelsea wanaonekana kubadilika zaidi , ile tabia ya kuwa na hamu ya kuwa na mpira wakati wote iko ndani ya kikosi chao, hali hii ilikuwa imeshapotea kwa sasa taratibu inaanza kurudi kwenye kikosi chao.

6: Kitu kikubwa kilichoongezeka msimu huu kwa kikosi cha Arsenal hasahasa kwenye mechi kubwa ni hamasa ya ushindi, wachezaji wengi wanajiamini kwenye mechi kubwa tofauti na misimu iliyopita. Ingawa nimewashuhudia kwa Liverpool, PSG na Chelsea kwenye mechi kubwa na hatuwezi tukaamini moja kwa moja kuwa wako tayari kushinda mechi kubwa kwa sasa, kwa sababu bado vipimo vikubwa vinakuja zaidi.

MUNGU AWABARIKI SANA.

No comments

Powered by Blogger.