KWA MAZOEZI HAYA YA SERENGETI BOYS, CONGO 'ANAKUFA' KWAO

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys wameendelea na mazoezi yao ya mwisho kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya Congo Brazaville kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana.


Tayari mashujaa hao wa Taifa wako Congo Brazaville na leo(Alhamisi) walikua wakijifua kwenye Uwanja wa Seminari Kuu ya Kumbukumbu ya Kardinali Emile Biayenda wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Brazzaville, Jamhuri ya Congo.

Serengeti Boys inajiandaa kucheza na vijana wa Congo, Jumapili ya Oktoba 2, 2016 kwenye dimba la Alphonse Massamba-Débat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville.





 (Picha na Alfred Lucas wa TFF).

No comments

Powered by Blogger.