KIPORO CHA YANGA NA JKT RUVU CHAPANGIWA TAREHE

Bodi ya ligi kuu ya soka Tanzania bara (TPLB) Imetoa ratiba ya michezo kadhaa ambayo ilikua haijapangiwa tarehe maalumu ya kuchezwa ukiwemo mchezo pekee wa kiporo mchezo namba 1 pbaina ya Yanga na JKT Ruvu.


Kiporo cha mchezo huo kilitokana na Yanga kukabiliwa na mchezo wa mwisho wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Sasa mchezo huo utapigwa Oktoba 26 jijini Dar es salaam ambapo Yanga itakua mwenyeji wa mchezo huo.

Mchezo mwingine namba 57 kati ya wenyeji Mwadui FC na Azam FC utachezwa tarehe 9 Novemba katika dimba la Mwadui Complex.

Tumekuweke hapa barua ya bodi ya ligi


No comments

Powered by Blogger.