KALI ZA LEO : KOCHA ALOYEWEKA HISTORIA TANZANIA AFARIKI DUNIA, RONALDO AZINDUA PAFUME YAKE

Karibu tena muda huu tuangalie kwa pamoja KALI ZA LEO ambazo zimejitokeza katika ulimwengu wa Soka kuanzia hapa nyumbani na barani Ulaya.



Hapa Nyumbani

● Aliyekuwa kocha wa zamani wa timu ya Mseto ya Morogoro Mohammed Msomali amefariki Dunia leo Mkoani Morogoro. Msomali ndiye aliyeipa timu ya Mseto Ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mwaka 1975 na kuifanya timu hiyo kuwa ya kwanza kutoka nje ya Dar es salaam kuchukua ubingwa huo.

● Timu ya Maji Maji ya Songea tayari imewasili jijini Dar es Salaam kwaajili ya mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Yanga SC, mechi itakayochezwa katika dimba la Uhuru jijini Dar.

● Klabu ya Azam FC ya Jijini Dar Es Salaam imeendelea kubaki jijini Mbeya baada ya kuibuka na ushindi jana dhidi ya Tanzania Prisons. Azam inatarajiwa kucheza dhidi ya Mbeya City siku ya Jumamosi.

Huko Ulaya leo

● Klabu ya Crystal Palace imekamilisha usajili wa kiungo wa zamani wa Arsenal na AC Milan Methieu Flamini kama mchezaji huru baada ya kuachwa na Arsenal baada ya kumalizika kwa msimu uliopita kwa mkataba wa mwaka mmoja.

● Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea Barcelona Neymar ameanza rasmi mazoezi na klabu yake ya Barcelona baada ya kutoka Brazil alikokua akiiwakilisha timu yake ya taifa.

● Mchezaji bora wa Ulaya Cristiano Ronaldo leo amezindua pafume yenye nembo yake inayojulikana kama CRISTIANO RONALDO LEGACY.


KWA LEO NI HAYO TU USIKU MWEMA

....S⚽KA LETU | JAMII YETU.

No comments

Powered by Blogger.