HIVI NDIVYO MASHUJAA KILIMANJARO QUEENS WALIVYOWASILI LEO (+PICHA)

Mabingwa wa michuano ya soka kwa  wanawake ukanda wa Afrika Mashariki timu ya taifa ya Tanzania bara upande wa wanawake maarufu kama Kilimanjaro Queens wamewasili jijini Dar.




Wakiwa na kombe lao la Ubingwa huo waliwasili majira ya jioni jijini Dar wakitokea Mwanza ambapo walilakiwa na mashabiki wa soka walioongozwa na katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF Mwesiga Celestine.

Mara baada ya kuwasili vijana hao walielekea moja kwa moja katika hoteli ya Court Yard iliyoko Upanga jijini Dar kwaajili ya hafla fupi pamoja na Waziri anayeshughulikia Michezo sanaa na wasanii Mheshimiwa Nape Nnauye.

Hizi hapa picha za mapokezi






No comments

Powered by Blogger.