HII HAPA RATIBA YOTE YA LIGI KUU TANZANIA BARA LEO

Mzunguko wa Tano wa ligi kuu Tanzania bara uatachezwa wikiend hii kwa timu zote 16 kujitupa uwanjani.


Moja kati ya matukio katika mechi zilizopita baina ya Azam na Simba
Pambano linalovuta hisia za wapenda Soka leo ni lile litakalopigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kati ya Azam FC na wekundu wa Msimbazi Simba.

Timu hizo mbili zinaongoza msimamo wa ligi hiyo zikiwa na pointi 10 kila moja na zikifanana kwa kila kitu.

Huko Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage wenyeji Mwadui FC watawakaribisha mabingwa watetezi Yanga pambano ambalo linapigwa Uwanja wa Kambarage kutokana na mazingira ya Uwanja wa Mwadui kutoruhusu mashabiki  wengi wanapocheza na Simba au Yanga.

Jijini Mbeya ni "Mbeya Derby" leo wenyeji Wa Uwanja wa Sokoine Prisons wataumana na wenzao Mbeya City mchezo unaogusa hisia za Wapenda Soka wa jiji hilo kutokana na upinzani mkali uliopo baina ya timu hizo.

Mjini Morogoro katika viunga vya Manungu Wenyeji Mtibwa Sugar watamkaribisha kocha wao wa zamani Mecky Maxime akiwa na kikosi cha Kagera Sugar.

Ruvu Shooting wao watakua Uwanja wa Mabatini pale Kibaha kumenyana na timu ngeni katika ligi hiyo Mbao FC ya Jijini Mwanza.

Maji Maji ya Songea wao watacheza na majirani zao timu ya Ndanda FC ya Mtwara mchezo unaotarajiwa kuchezwa katika dimba la Maji Maji pale Songea.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa michezo miwili wakati African Lyon watakapocheza na Toto African huku Stand wakicheza na JKT Ruvu ya Pwani.

No comments

Powered by Blogger.