BAADA YA KUIBUKA NA USHINDI MNONO JANA SASA MAN UNITED KUKUTANA NA MAN CITY HATUA INAYOFATA

Usiku wa jana Manchester United ilisahau adha ya kufungwa mechi 3 mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-1 katika michuano ya kombe la Ligi nchini England.


Man United iliifunga Northampton jana kwa magoli ya Michael Carick,Ander Herrera na Marcus Rashford na kutinga katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ambayo bingwa wake mtetezi ni Manchester City.

Usiku huo wa jana katika michuano hiyo pia Manchester City iliinyuka Swansea bao 2-1, Sunderland ikaifunga QPR bao 2-1.

Matokeo mengine ya jana Bristol City iliifunga Fulham bao 2-1, Huku Southampton ikainyuka Crystal Palace bao 2-0.

West Ham ikaifunga Accrington bao 1-0, Wakati Hull City wakaifunga Stoke City bao 2-1 na Tottenham wakaikandamiza Gillingham bao 5-0.

Baada ya mechi za jana Ratiba ya Hatua ya 16 bora ilipangwa na hizi ndiyo mechi zilivyopangwa


  • West Ham vs Chelsea
  • Manchester United vs Manchester City
  • Arsenal vs Reading
  • Liverpool vs Tottenham
  • Bristol City vs Hull City
  • Leeds United vs Norwich City
  • Newcastle United vs Preston North End
  • Southampton vs Sunderland
MECHI HIZI ZITACHEZWA WIKI INAYOANZIA TAREHE 24 OKTOBA 

No comments

Powered by Blogger.