BAADA YA KICHAPO KAGERA JULIO ATISHIA KUACHANA NA SOKA LA BONGO
Kocha mkuu wa Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu Julio ametishia kuachana na soka la bongo kwa kile alichoeleza kuwa Marefa kushindwa kumudu sheria 17 za soka.
Julio alisema hayo baada ya timu yake ya Mwadui kufungwa bao 1-0 na Kagera Sugar katika pambano la ligi kuu Tanzania bara lililopigwa katika dimba la Kaitaba jana.
Mchezo huo ulikua wa kwanza katika uwanja huo kufatia matengenezo makubwa pamoja na uwekaji nyasi bandia katika uwanja huo.
Julio analalamikia maamuzi ya refa ambaye anasema alitoa maamuzi ya kuikandamiza timu yake na kuwanyima penati 3 za wazi huku waamuzi wa pembeni wakiwaambia wachezaji wake kwamba lazima wafungwe katika mchezo huo kabla haujaanza.
Julio alisema hayo alipohojiwa na kituo kimoja cha radio baada ya mchezo huo na akasema haoni haja ya kuendelea kupoteza nguvu zake kwa soka ambalo linaharibiwa na watu wachache.
Katika mechi zingine hiyo jana Mbao FC ikiwa nyumbani ililala kwa bao 4-1 toka kwa Mbeya City,Mtibwa Sugar wakaifunga Majimaji wakati African Lyon ikalazimishwa sare ya bila kufungana na JKT Ruvu

No comments