ADEBAYOR AKANUSHA KUKATALIWA KUSAJILIWA LYON KISA POMBE NA SIGARA
Nahodha wa zamani wa Togo na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal,Man City na Tottenham Emmanuel Adebayor ameibuka na kukanusha uzushi uliozagaa jana.
Kulikua na taarifa kwamba Adebayor ameshindwa kujiunga na Olympic Lyon ya Ufaransa kisa Aliagiza pombe na sigara wakati wa mazungumzo na wawakilishi wa klabu hiyo ili kusaini mkataba wa kuichezea.
Mshambuliaji huyo ambaye yuko huru hivi sasa baada ya kuachwa na Crystal Palace ametanabaisha kwamba jambo hilo ni uzushi na halina ukweli wowote ni uzushi tu uliotungwa na gazeti moja huko Ufaransa.
Adebayor ameeleza hali ilivyokua "Lyon ilituma ndege kunifata Togo na wakati wa mazungumzo niliagiza maji tu na sio wisky na sigara kama ilivyoandikwa ila kilichonifanya nisisajiliwe ni baada ya kuchelewa kufika huku Lyon wakiwa wameshamsajili kijana chipukizi wa kuziba nafasi ya Lacazette ambaye ni mgonjwa"
Kocha alitaka kujua mambo mengi kuhusu mimi tangu nilipokua Crystal Palace pia akataka kujua kama ningecheza kama akiba ya kijana aliyesajiliwa jambo ambalo niliona si busara kwangu"
Alimaliza kusema Adebayor.
Baada ya kushindikana sasa kujiunga na Olympic Lyon bado mshambuliaji huyo ana imani atapata timu nyingine.

No comments