YANGA KUKAMILISHA RATIBA LEO INACHEZA NA TP MAZEMBE LUBUMBASHI

Mabingwa wa Tanzania bara Yanga leo wanacheza mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba dhidi ya TP Mazembe mjini Lubumbashi.


Mechi hiyo ya Robo fainali katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika inachezwa leo kuanzia majira ya saa 9 na nusu Alasiri kwa saa za hapa nyumbani na ni ya kukamilisha ratiba tu kwani Tayari TP Mazembe wameshafuzu hatua ya nusu fainali huku Yanga ikiwa imeshazika matumaini ya kutinga nusu fainali.

Kikosi cha yanga jana kilifanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea katika mchezo wa leo katika uwanja utakaopigwa mchezo huo yani  Stade de TP Mazembe.

Wachezaji walikuwa na ari na morali ya juu mazoezini.
Hakuna majeruhi yeyote katika kikosi cha yanga kilichopo Lubumbash.

No comments

Powered by Blogger.