MANCHESTER UNITED KUIKARIBISHA EVERTON LEO OLD TRAFFORD

Leo katika jiji la Manchester kutapigwa mchezo maalumu wa kumuenzi nahodha wa United na England Wayne Rooney.



Man United itaikaribisha Everton katika mchezo huo wa kumuenzi Wayne Rooney ambaye amecheza katika timu mbili tu mpaka sasa yani Everton na Manchester United.

Huu ni mwaka wa 12 tangu Rooney alipojiunga kuichezea Man United akitokea Everton huku pesa zitakazopatikana katika mchezo huo zikitarajiwa kuendeleza Wayne Rooney Foundation.

Mchezo huo pia utakua wa kumkaribisha kocha Jose Mourinho katika dimba la Old Trafford kama kocha mkuu ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipochukua kazi ya kuinoa

Pia utakua mchezo wa mwisho wa maandalizi kwa Man United kabla ya kuikabili Leicester City katika mechi ya ngao ya hisani.

Pambano hilo litaanza saa 4 usiku na kurushwa na vituo mbalimbali vya luninga na kwa mara ya kwanza kupitia ukurasa wa Facebook wa Wayne Rooney na Ule wa Manchester United lakini hapa nyumbani tunaweza kuiona mechi hiyo kupitia Azam TV (MUtv)

No comments

Powered by Blogger.