LIGI KUU YA ENGLAND MABINGWA LEICESTER CITY KUANZA KUTETEA UBINGWA NA WAGENI HULL CITY

Miezi mitatu ya tambo na usajili mbalimbali kwa klabu za ligi kuu nchini England inakamilishwa leo kwa ufunguzi wa ligi hiyo inayopendwa zaidi Duniani.


Leo Jumamosi michezo kadhaa ya ufunguzi wa ligi hiyo itapigwa huku mabingwa watetezi Leicester City wao watafungua utepe wa ligi hiyo kwa kucheza na Hull City iliyopanda daraja mechi inayotarajia kuanza majira ya saa 8 na nusu mchana.

Mechi ya mwisho leo itakua Sunderland na Manchester City mechi ya kwanza kwa Pep Guadiola katika ligi kuu ya England akiwa na kikosi cha Man City pia itakua mechi ya kwanza ya ligi kwa kocha David Moyes ndani ya Sunderland mechi itakayopigwa saa moja na nusu usiku.

RATIBA KAMILI

2:30 PM - Hull City vs Leicester City
5:00 PM - Burnley vs Swansea City
5:00 PM - Crystal Palace vs West Bromwich Albion
5:00 PM - Everton vs Tottenham Hotspur
5:00 PM - Middlesbrough vs Stoke City
5:00 PM - Southampton vs Watford
7:30 PM - Manchester City vs Sunderland

NOTE: MUDA NI KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI

No comments

Powered by Blogger.