KAZI INAANZA LEO ENGLAND, NI MAN UNITED VS LEICESTER CITY NGAO YA JAMII

Ufunguzi wa pazia la msimu mpya wa ligi kuu nchini England utakua leo katika dimba la Wembley kati ya Manchester United na Leicester City.


Leicester City ndiyo mabingwa wa ligi hiyo msimu uliopita huku Man United wao ndiyo mabingwa wa kombe la FA na wanakutana katika mchezo wa ngao ya jamii leo ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza rasmi kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini England itakayoanza wikiend ijayo.

Man United ikiwa na kocha mpya Jose Mourinho itaingia katika mchezo wa leo ikitaka kuchukua ngao hiyo kwa mara ya 21 baada ya kufanya hivyo mara 20 katika historia ya mchezo huo wakati Leicester City wakitaka kuchukua kwa mara ya kwanza kama walivyofanya msimu uliopita kwa kuchukua ubingwa wakati hakuna aliyewapa nafasi.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na kurushwa na vituo mbalimbali vya luninga duniani.

Ni mechi ambayo tutashuhudia kasi kubws katika safu ya ushambuliaji kwa timu zote mbili Man United ikiwatumia Ibrahimovic,Rooney na Antony Martial wakati Leicester wao wana Jarmie Vardy,Ahmed Mussa na Ryad Mahrez.

Kwa upande wa ulinzi kila timu ina kipa bora United wakiwa na David De Gea huku Leicester City wao wakiwa na mtoto wa gwiji wa zamani wa Man United Kasper Schmeichel.




No comments

Powered by Blogger.