KARIBU TENA RANGERS, REJESHA MSISIMKO WA LIGI KUU SCOTLAND

Ligi kuu ya soka ya Scotland, Scottish Premeirship (SPFL) imerudi kivingine kuanzia leo, ni msimu ambao Rangers imerejea katika ligi hiyo baada ya kukaa katika madaraja ya chini kwa miaka kadhaa baada ya kushushwa daraja.


Leo wakicheza mchezo wa kwanza Rangers wametoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Hamilton Academical.

Ikumbukwe kwamba Rangers wamerudi ligi kuu kwa nguvu baada ya kuwasajili Clint Hill, Joey Barton na Niko Kranjcar, wachezaji ambao wana uzoefu wa kucheza miaka mingi kwenye ligi kuu ya England wakiwa na klabu tofauti.

Inatarajiwa kwamba Rangers wataleta upinzani mkubwa kwa mahasimu wao wa kudumu Celtic, ambao wanatoka pamoja mji wa Glasgow na kuunda derby ya Old Firm.

Kushushwa daraja kwa Rangers mwishoni mwa msimu wa 2011/2012 kutokana na kufilisiwa, kuliwapa urahisi Celtic kutawala ligi, ukizingatia kuwa timu hizo mbili ndizo zenye nguvu na mafanikio makubwa kuliko nyingine nchini Scotland.

Kinachosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka wa Scotland ni je, Celtic wataendeleza utawala, au Rangers watakuja kutibua ufalme huo?

..Na Jerry Bilinje : Wapenda Soka Tanzania

No comments

Powered by Blogger.