SIMBA YAMTANGAZA KOCHA WA ZAMANI WA CAMERON KAMA KOCHA WAKE MKUU
Katika kurudisha makali yake wekundu wa msimbazi Simba wamemtangaza aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Cameroon na Azam FC Joseph Marius Omog kama kocha wake mpya.
Omog raia wa Cameroon aliyewahi kuifundisha Azam Fc kabla hajatimuliwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa Simba ambayo kwa muda mrefu imekaa bila ya kocha.
Rais wa Simba Evance Aveva amemtambulisha kocha huyo mbele ya waandishi wa habari mchana huu jijini Dar Es Salaam akimtambulisha pia Katibu mkuu mpya wa klabu hiyo Patrick Kahemele.
Omog akiwa Azam FC alifanikiwa kuiongoza kwa msimu mmoja na nusu ikishinda mechi 30 kati ya 55 za mashindano yote, sare 14 na kufungwa mara 11.
Mwalimu huyo aliyeipa Leopard FC ya Kongo Brazaville Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2012, enzi zake alichezea Yaounde na ni mwalimu wa kiwango cha juu cha ufundishaji soka na mazoezi ya viungo aliyehitimu vizuri mafunzo yake katika Chuo cha Vijana na Michezo, INJS mjini Yaounde, Cameroon.
Alikwenda kujiendeleza kielimu nchini Ujerumani na kwa pamoja na Pierre Njili na Martin Ndtoungou walipata Stashahada za ukocha na leseni za UEFA daraja la B mwaka 1987.
Omog aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Mjerumani, Winfried Schafer katika timu ya taifa ya Cameroon na baadae akapewa nafasi ya kocha mkuu wa nchi hiyo inayoheshimika kwa soka barani Afrika.

No comments