SENTENSI ZA TAJIRI MOHAMED DEWJI WAKATI AKITANGAZA MPANGO WA KUINUNUA KLABU YA SIMBA

Mkurugenzi mtendaji na Rais wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) ambaye pia ni bilionea kijana Afrika Mohammed Dewji ‘MO' amezungumzia mpango wake wa kuinunua Simba.


Mohammed Dewji ameweka wazi mpango wake wa kutaka kununua hisa asilimia 51 za
Simba na faida watakayopata wanachama wa Simba baada ya
Mohammed Dewji kuinunua klabu hiyo.

"Sababu za Simba kutofanya vizuri ni kutokana na bajeti, mfano Yanga bajeti yao inaweza kufikia bilioni 2.5 sawa labda na Azam FC wakati bajeti ya Simba inaweza kuwa nusu ya bajeti za washindani wake."

"Simba kwa sasa haihitaji mdhamini ili kuweza kujiendesha au kumtegemea kwa maana mpira unahitaji pesa na sio mdhamini atakayetoa milioni 400 au chini ya hapo."

"Wanachama wa Simba wa muda mrefu watapewa hisa bure na sio kujivunia kadi ya uanachama isiyoingiza kitu chochote, utakuwa na uwezo wa kuuza hisa zako au kununua nyingine kama utahitaji."

"Simba kwa sasa inatakiwa iwe mbali ya hapo ilipo kwani sasa inatimiza miaka 80 toka ianzishwe, lakini haina hata uwanja wa mazoezi tumezidiwa hata na Azam FC wameanza juzi."

 "Nilijitoa African Lyon ni baada ya kwenda uwanjani na kuona timu haina mashabiki mpira unahitaji mashabiki, hata Simba kama isingekuwa na mashabiki nisingeingia mpira unahitaji mashabiki, kuhusu Singida United niliidhamini ikaingia Ligi Kuu zikaanza siasa nikaamua kujitoa"

>>>"Mimi dhamira yangu sio kupata pesa kutoka Simba, nashukuru Mungu amenijalia sana nina biashara zaidi ya 100, tumeajiri watu 28,000 na tutaendelea kuajiri zaidi, dhamira yangu ni kuona Simba inasonga mbele zaidi"

No comments

Powered by Blogger.