PEP GUADIOLA USO KWA USO NA BAYERN MUNICH LEO KATIKA MECHI YA KIRAFIKI

Siku chache baada ya kuondoka katika kikosi cha Bayern Munich kocha mpya wa Manchester City atarudi katika dimba la Allianz Arena na kikosi cha Man City.


City na Bayern zitakutana katika mechi hiyo ya kirafiki maalumu kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Huo utakua mchezo wa kwanza wa Pep Guardiola akiwa na kikosi cha City huku Wapenda Soka wengi wakitaraji kuona vijana wakipewa nafasi katika kikosi cha Pep Guadiola leo.

Guadiola aliifundisha Bayern Munich misimu mitatu akifanikiwa kushinda mfululizo ubingwa wa Bundesliga miaka yote mitatu na kutolewa katika nusu fainali mara 3 katika ligi ya mabingwa Ulaya.

Mechi hii inatarajiwa kuanza saa 3 na nusu usiku kwa saa za hapa nyumbani Tanzania

No comments

Powered by Blogger.