MTIBWA SUGAR YAWASAJILI MANDAWA NA PONERA

Wakata miwa wa mjini Morogoro Klabu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kuinasa saini ya mshambulijai wa Timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Mwadui FC Rashid Mandawa.

 Mandawa amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga katika klabu hiyo ya Manungu Complex habari ambayo imethibitishwa na Mtendaji mkuu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser ambaye amemtaja pia beki wa Ndanda FC  Cassian Ponera kusajiliwa na Mtibwa Sugar kuziba nafasi iliyoachwa na Endrew Vicent aliyetimkia Yanga.

Mtibwa Sugar iliyomaliza katika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi hiyo msimu uliopita itajengwa upya na kocha Salumu Mayanga ambaye msimu uliopita alikua akiinoa Prisons ya Mbeya.

Mtibwa Sugar mabigwa wa 1999 na 2000 wa Ligi ya Vodacom Tanzania wameanza maandalizi ya msimu ujao wakiweka kambi yao Jijini Dar es Salaam kabla ya kurudi Manungu kwenye kambi yao ya siku zote.
Mandawa


No comments

Powered by Blogger.