KATIKA SIKU AMBAYO MESSI ANANUSURIKA KUFUNGWA JELA,RONALDO ANAIPELEKA URENO FAINALI EURO 2016

Siku ya tarehe 6 Julai imetawaliwa na Habari mbili kuu zinazowahusu wacheza soka bora kabisa kuwahi kutokea Duniani yani Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

 Wakati Lionel Messi akikutwa na hatia ya kukwepa kulipa kodi na kuhukumiwa kifungo cha miezi 21 Jela hatimaye kuepuka adhabu hiyo kwa kulipa faini yeye na baba yake, Ronaldo yeye aliweka rekodi mpya katika michuano ya Euro akifunga bao 1 na kutoa pasi moja ya goli.

Akiiongoza Ureno waliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Wales katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo inayoendelea nchini Ufaransa.

Ronaldo alifunga bao la kwanza kwa timu yake kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona iliyochongwa na beki wa pembeni Raphael Guerreiro dakika ya 50 na dakika 3 baadae Ronaldo alimtengenezea Luis Nani aliyefunga bao la pili ambalo lilidumu mpaka mwisho.

Kwa matokeo hayo Ureno inatinga fainali itkayochezwa tarehe 10 ambapo itakutana na mshindi wa mechi kati ya Wenyeji Ufaransa na mabingwa wa dunia Ujerumani mchezo utakaopigwa leo Alhamisi.

No comments

Powered by Blogger.