JERRY MURO ASEMA WANAOWEZA KUNISIMAMISHA KAZI NI YANGA TU, APINGA ADHABU ALIYOPEWA

Mkuu wa habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro amesema hatambui adhabu iliyotolewa na TFF ya kufungiwa mwaka mmoja na kulipa faini ya milioni 3.
Akizungumza na moja ya radio maarufu nchini Tanzania Muro ambaye hatakiwi kujishughulisha jambo lolote la soka mpaka adhabu yake itakapoisha amesema moja ya sababu inayomfanya asikubali adhabu hiyo ni kushindwa kusikilizwa wakati maamuzi hayo yanatolewa jana.

Pia Muro amesema "Yeye ameajiriwa na Yanga hivyo basi wenye mamlaka ya kumfuta kazi au kumsimamisha ni Yanga wenyewe na yeyote/taasisi nyingine yeyote.

Jerry alihukumiwa na kamati ya maadili ya TFF kutojihusisha na soka kwa muda wa mwaka mmoja kutokana na 
- Kukaidi agizo la kulipa faini tangu mwezi Mei mwaka jana.
- kuipinga TFF Pale TFF walipotaka jukwaa la Simba lililoko uwanja wa taifa lisikaliwe na washabiki wa Yanga katika mechi ya yanga dhidi tp mazembe june 27 mwaka huu. 
- kutamka maneno ya kichochezi kwenye vyombo vya habari.


No comments

Powered by Blogger.