GONZALO HIGUAIN AKABIDHIWA JEZI NAMBA 9 JUVENTUS

Mabingwa wa Italia Juventus wamekamilisha usajili wa Gonzalo Higuain kwa kumkabidhi jezi namba 9.


Mshambuliaji huyo Raia wa Argentina amesajiliwa na Juventus akitokea klabu ya Napoli kwa moja kati ya usajili uliovunja rekodi wa paundi milioni 76 akisaini mkataba wa miaka mitano.

Gonzalo Higuain  mwenye miaka 28 anatarajia kupata kiasi cha paundi milioni 6.3 kwa mwaka baada ya kukatwa kodi.

Gonzalo Higuain amechukua jezi hiyo ambayo awali ilikua ikivaliwa na mshambuliaji Alvaro Morata ambaye amerudi Real Madrid.

No comments

Powered by Blogger.