EURO 2016 : MIKWAJU YA PENATI YAIPELEKA URENO YA RONALDO NUSU FAINALI
Mechi ya kwanza ya robo fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya Euro 2016 baina ya Ureno na Poland imeamuliwa na changamoto ya mikwaju ya penati.
Wababe katika mchezo huo ni Ureno wakiongozwa na Cristiano Ronaldo wakiibuka na ushindi wa penati 5-3 baada ya mchezo huo kumalizika matokeo yakiwa ni sare ya bao 1-1.
Nahodha wa Poland Roberto Lewandowski alitangulia kufunga bao la mapema kabisa dakika ya 2 tu ya mchezo baada ya kuwahadaa mabeki wa Ureno na kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa Ureno.
Dakika ya 33 ya mchezo chipukizi Renato Sanchez ambaye msimu ujao atakipiga ndani ya Bayern Munich aliisawazishia Ureno bao akipokea pasi ya kisigino ya Luis Nani.
Mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yalibaki sare ya 1-1 hata zilipoongezwa dakika 30 bado hakukuwa na tofauti ndipo changamoto ya mikwaju ya penati ikatumika.
Wachezaji wote wa Ureno waliopiga penati hizo walifunga ikiwemo penati ya ufunguzi ya nahodha Cristiano Ronaldo,Renato Sanchez,Joao Mortinho,Nani na penati ya ushindi aliyopiga Ricardo Quaresma.
Poland wao walikosa penati moja katika penati 4 walizopiga Jacub Blaszczykowski akiwa ndiye aliyekosa penati ikidakwa na kipa wa Ureno Rui Patricio.
Kwa matokeo haya Ureno sasa wanatinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo wakisubiri mechi zingine za Robo fainali leo kesho na keshokutwa.

No comments