LICHA YA KUINGIZA BURE MASHABIKI,YANGA YAKUMBANA NA KICHAPO TAIFA
Pambano hilo lilichezwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam halikua na kiingilio kwa mashabiki waliojitokeza kulitazama na hivyo kupelekea uwanja huo wenye uwezo wa kujaza mashabiki 60,000 kujaa
Mpaka mapumziko Hakuna timu iliyofanikiwa kuliona lango la timu pinzani na kupelekea matokeo kubaki bila bila.
Kipindi cha pili Tp Mazembe walionekana kuwa bora zaidi na kuwazidi ujanja Yanga wakipata bao pekee dakika ya 74 likifungwa na mlinzi wa Mazembe raia wa Congo Merveille Bope Bokad74
Kwa matokeo hayo Tp Mazemne wanaongoza kundi A wakiwa na pointi 6 na Yanga ni ya mwisho.


No comments