KUINGIA UWANJANI BURE KWAIGHARIMU YANGA YATAKIWA KULIPA MILIONI 530.
SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka nchini (TFF), limeitaka Yanga kulipa fidia ya gharama za mchezo wake wa leo jioni katika hatua makundi dhidi ya TP Mazembe kiasi cha Sh milioni 530.
Hii inatokana na hatua ya Yanga kufuta kiingilio katika mchezo wao huo unaotarajiwa kuchezwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Katika kikao chao cha jana kilichofanyika kwenye hoteli ya Coral Beach jijini na kukutanisha maofisa wa CAF, uongozi wa TFF, Polisi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na viongozi wa Yanga wakiongozwa na Katibu mkuu wa klabu hiyo, Baraka Deusdetit wametakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kama gharama za mchezo.
Makato katika mchezo huo wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho asilimia 15 ya fedha hizo zitaenda CAF, asilimia 15 nyingine gharama ya uwanja, TFF asilimia tano, Baraza la Michezo la Taifa (BMT), asilimia 10, na Chama cha soka Dar es Salaam (DRFA) asilimia tano.
Tayari Yanga ilikuwa imechapisha tiketi 31,000 ambazo zingeuzwa kwa Sh7,000 ambazo zingeingiza Sh 217,000,000 huku zile za Sh 25,000 zilikuwa zimechapishwa tiketi 8,200 zingeingiza Sh milioni 205 huku VIP zilikuwa tiketi 5,000 ambazo zingeingiza Sh milioni 150 jumla ya fedha zote ambazo zingepatikana katika mchezo huo ni Sh milioni 572.
Pia Yanga wametakiwa kuingiza mashabiki wasiozidi 40,000 wakizidi kiwango hicho mchezo huo utafutwa na Yanga watalazimika kuwajibishwa.
Yanga wanadai wana mdhamini mpya amabye wangependa aone jinsi uwanja utakavyojaa ili ashawishike kuingia nao mkataba wenye tija kwa klabu hiyo.
Kwa upande wa Ofisa habari wa Yanga, Jerry Muro jana alisema kuwa CAF imewataka kudhibiti mashabiki wao na kwamba watakaoingia uwanjani ni watu 40,000 tu.
“Mashabiki wawahi uwanjani, Kamisaa wa mchezo kasema ikifika idadi ya watu 40,000 geti litafungwa na watakaoingia wataingia wengine watatusamehe, wakizidi mashabiki 40,000 mchezo utafutwa, na sisi tunazingatia hilo, na hiyo ni kutokana na hali ya usalama,”alisema Muro.
Kufuatia hali hiyo, Yanga watalazimika kudhibiti kiwango cha mashabiki wao ili kuepuka mchezo huo kufutwa na wao kuchukuliwa hatua za kisheria.

No comments