KOCHA WA ZAMANI VITAL O YA BURUNDI KUINOA MBAO FC YA MWANZA

Na Alexander Sanga,Mwanza

Timu ya Mbao Fc ya wilayani Ilemela mkoani hapa  iliyopanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu mpya wa 2016/17,jimeingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha Etienne Ndairagije ambaye ni raia wa Burundi na kocha wa zamani ya Vital O' ya nchini Burundi



Akizungumza na gazeti hiliMwenyekiti wa Mbao Fc Solly Njashi amesema kuwa wameingia mkataba na kocha huyo baada ya kujiridhiisha na tawasifu yake (CV). Njashi amesema timu hiyo itaonyesha upinzani mkubwa sana katika ligi kuu msimu huu mpya na ameomba wana Mwanza waungane katika kuhakikisha wanashangilia timu yao iweze kufanya vyema.

Naye kocha mkuu wa mpya wa Mbao Fc, Etienne Nagiragije, amesema kuwa atatumia falsafa yake ya kutumia vijana zaidi na wazoefu wachache katika timu yake ili kuleta ushindani katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
Nagiragije ameuomba uongozi wa Mbao fc usijaribu kuingilia majukumu yake bali umpe uhuru Zaidi kocha huyo afanye kazi kwa bidii na amesema katika suala la usajili atahakikisha wanasajili wachezaji vijana na wenye vipaji vya hali ya juu

Pia kocha huyo amesema kuwa atahitaji uhuru zaidi wa maamuzi katika benchi lake la ufundi ili kufanya usajili unaookidhi na kuwaomba viongozi wa Mbao Fc kutoingilia maamuzi yake ya kiufundi.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha soka wilaya ya Ilemela(IDFA)Juma Msaka, amesema kuwa amefurahishwa sana wilaya yake kwa mara ya kwanza katika historia ya soka kusimamisha timu itakayoshiriki Ligi Kuu na kuahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Mbao Fc ili timu hiyo
ishindane kikamilifu Ligi itakapo anza.


No comments

Powered by Blogger.