JEURI YA PESA : YANGA YAFUTA VIINGILIO SASA MECHI YAO YA KESHO NA TP MAZEMBE HAKUNA KIINGILIO

Mabingwa wa Tanzania bara Yanga wamekata mzizi wa fitina uliotanda kuhusu haki za matangazo ya mchezo wao wa kombe la shirikisho dhidi ya TP Mazembe kwa kufuta kabisa viingilio katika mchezo huo.


Kulizuka mgongano wa mawazo baina ya Yanga na shirikisho la soka Nchini Tanzania TFF na lile la Afrika CAF kuhusu mchezo huo Yanga wakitaka kumiliki kila kitu kinachohusu mchezo huo zikiwemo haki za matangazo huku CAF na TFF wakiipa Azam Tv haki za kurusha moja kwa moja mchezo huo.

Tayari Yanga walishatangaza viingilio vya mchezo huo ambavyo vilikua ni 7,000 kama kiingilio cha chini na hivi sasa kiingilio hicho kimefutwa na itakua bure kabisa.

Mchezo utaanza saa 10 Alasiri katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam uwanja wenye uwezo wa kubeba watazamaji 60,000

Kwa hali ilivyo kama mashabiki wataingia bure uwanjani basi Yanga itawabidi kugharamia kila kitu katika mchezo huo pesa ambazo zitatoka katika akaunt zao na sio viingilio kama ilivyokua siku za nyuma.

No comments

Powered by Blogger.