COPA AMERICA: URUGUAY YAANGUKIA PUA KWA MEXICO, VENEZUELA YAIADHIBU JAMAICA

Mashindano ya kombe la mataifa ya America Yanayojulikana zaidi kama Copa America yaliendelea jana kwa mechi 2 kupigwa katika viwanja viwili tofauti nchini Marekani.


Mexico ikiwa katika kiwango bora kabisa iliiadhibu Uruguay bao 3-1 moja kati ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Magoli ya Maxico yaliwekwa kimiani na Rafael Maquez, Hector Herrera na goli la kujifunga la Alvaro Pereira wakati goli la kufutia machozi la Uruguay likiwekwa kimiani na mlinzi Diego Godin.

Katika mechi ya awali Venezuela waliinyuka Jamaica bao 1-0 goli pekee la dakika ya 15 tu ya mchezo likifungwa na mshambuliaji Josef Martinez

Kwa matokeo hayo Mexico wanaongoza kundi C wakiwa na pointi 3 sawa na Venezuela huku Jamaica na Uruguay wakishika mkia

Mechi za michuano hiyo zitaendelea leo kwa mechi mbili za kundi D ambapo Panama watacheza na Bolivia saa 8 usiku na Argentina wataumana na Chile saa 11 Alfajiri kesho kwa saa za Afrika Mashariki.


No comments

Powered by Blogger.